NA MWANDISHI WETU SUPER SOLOTZ
KUNDI la kudansi la WD lenye maskani yake Keko Machungwa, Dar es Salaam, limeibuka kuwa mabingwa wa mashindano ya Dance 100% baada ya kuwabwaga wenzao katika fainali zilizofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco, Oysterbay, jijini juzi na hivyo kuondoak na kitita cha Sh milioni tano kutoka kwa wadhamini wakuu, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Washindi wa pili lilikuwa ni kundi la Timu ya Shamba, wakati Best Boys Kaka Zao, walishika nafasi ya tatu, ikiwa ni baada ya mchuano mkali miongoni mwa makundi matano yaliyokuwa yametinga fainali.

Baada ya kutangazwa washindi, mashabiki waliofurika kwenye viwanja hivyo, waliripuka kwa shangwe wakionyesha kuridhishwa na uamuzi chini ya majaji, dansa Super Nyamwela, wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Queen Darleen na Shettah.

Akizungumza baada ya kutwaa ubingwa na kukabidhiwa kombe, mmoja wa madansa wa WD, Isdory Cosmas, alisema: “Tumefurahi sana kuwa washindi wa mashindano haya, waamuzi wametenda haki kwani tulistahili kushinda kutokana na uchezaji wetu ambao haukuwa na komedi wala mbwembwe kama ilivyokuwa kwa makundi mengine.”

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,ambao ndiyo wadhamini wakuu kwa mwaka wane mfululizo wa mashindano haya alitoa pongezi kwa kundi la WD kwa kuibuka washindi, lakini pia kwa waandaaji EATV waliofanya hivyo kwa mwaka wa nne mfululizo sasa, akiyataka makundi yaliyotoka kappa kujipanga kwa ajili ya mwakani.

“Vodacom Tanzania tutaendelea kudhamini mashindano haya mwakani kwani kadri ya miaka inavyokwenda, yamezidi kuwa na msisimkoa. Nitoe wito kwa wasanii kuwashika mikono hawa vijana waweze kuendeleza vipaji vyao na mwisho wa siku, kupata ajira ya kuwawezesha kuendesha maisha yao,” alisema Nkurlu.

Alisema kuwa sanaa ikitiliwa mkazo na kufanyika kwa umakini itawawezesha vijana wengi kujiajiri na kujipatia kipato cha kuwawezesha kuendesha maisha yao vizuri “Vodacom tayari tunatambua kuwa sanaa na michezo inaweza kuinua  hali ya maisha ya vijana kwa kupunguza tatizo la ajira ndio maana kampuni yetu imejikita kudhamini mashindano mbalimbali ya sanaa ikiwemo shindano hili la Dansi 100% na daima tutaendelea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na tatizo la ajira kwa vijana.

Nkurlu alisema ushahidi upo wa vijana wengi hapa nchini ambao miaka michache iliyopita hawakuwa na maisha ya uhakika lakini hivi sasa  wanaendesha maisha yao vizuri kutokana na kazi za sanaa wanazozifanya baadhi yao wakiwa ni wanamuziki na wengine wachezaji wa michezo mbalimbali. 
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tano(5) John Aron ambaye ni kiongozi wa kundi la  WD kutoka Keko Machungwa jijini Dar es Salaam,lililoibuka mabingwa wa mashindano ya Dance 100% baada ya kuwabwaga wenzao katika fainali zilizofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini mwishoni mwa wiki,shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Nyomi ya wapenzi wa dansi walivyofurika katika viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Ambapo kundi la  WD kutoka Keko Machungwa jijini lilibuka  mabingwa wa mashindano ya Dance 100% 2015. shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Kombe pamoja na kitita cha shilingi Milioni tano(5) zilinyakuliwa na kundi la  WD kutoka Keko Machungwa jijini Dar es Salaam na kutawazwa  mabingwa wa mashindano ya Dance 100% 2015 chini ya  EATV na Vodacom Tanzania.

 Mastaa hawakukosekana Bi.Almas”Mwasiti”ndani ya shindano la kukata na shoka la Dance 100% 2015 lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es salaam na kundi la  WD kutoka Keko Machungwa jijini kutawazwa  mabingwa wa mashindano hayo chini ya  EATV na Vodacom Tanzania na kujinyakulia Kombe pamoja na kitita cha shilingi Milioni tano(5) toka Vodacom Tanzania.
Makundi yaliyoshiriki katika shindano la dance 100% 2015 mwishoni mwa wiki yakichuana vikali katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam,Ambapo kundi la  WD kutoka Keko Machungwa jijini kutawazwa  mabingwa wa mashindano hayo chini ya  EATV na Vodacom Tanzania na kujinyakulia Kombe pamoja na kitita cha shilingi Milioni tano(5) toka Vodacom Tanzania.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top