MAFURIKO YA LOWASSA ARUSHA JIJI LASIMAMA. MZEE KINGUNGE AFUNGUKA MAZITO

                                                                          wananchi wafurika na shuhuri nyingi kusimama
Edward Ngoyai Lowassa na Godbless Lema wakiwasili katika viwanja vya Sinoni Unga Ltd leo Alhamisi 8/10/2015












































KADA Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi CCM,Kingunge Ngombale –Mwiru ambaye amekiaga chama hicho ,ameendelea kukitolewa lawama cha hicho kusema CCM pumzi yake imefikia mwisho na haikitaki kupewa tena dhamana ya kuongoza nchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
     
Akizungumza  wakati wa Kampeni za kumnadi Mgombea Urais kupia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vya Ukawa,Edward lowassa zilizofanyika leo Arusha Mjini na kushuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao uliosababisha shughuli nyingi kusimama.
       Ambapo Kingunge  amedai chama chake hicho kilichomlea kimechoka na hakina nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania kwa lindi kubwa la umasikini.
      Amesema CCM anayoijua yeye tangu ilipokuwa TANU ilikuwa yenye misingi na kuweka mipango ya kumletea maendeleo moja kwa moja lakini amedai CCM hile sio hii ya sasa kwani hii ya sahivi imetekwa na watu wachache wenye kujali maslahi binafsi na sio kumleta maendeleo mtanzania.
       Kingunge huku akishangiliwa kwa nguvu,ammshukia pia Rais Jakaya Kikwete kwa kusema utawala wake umeua uchumi wanchi,
“Leo uchumi wa nchi umeporomoka,wakati Mkapa anamwachia nchi Kikwete uchumi ulikuwa kwenye hali nzuli,lakini baada ya kuingia yeye uchumi wan chi umedorola huku umasikini unazidi kuwa mkubwa kwa watanzania’
  SUMAYE ANENA.
Kwa upande wake Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu,Fredrick Sumaye amewataka watanzania kutomchagua Mgombea wa Urais kupitia CCM John Magufuli kwa kuwa mgombea huyo anamaamuzi ya kukurupuka na ambaye asiyekubali kushaulika jambo ambalo  amewasihii Watanzania kuwa watakuja juta.
Sumaye amesema hata  wizara alizopewa  Magufuli kuongoza ameonyesha utendaji wa kibabe usiofuata utu na uzalendo kwa watanzania.
  LOWASSA ANADI SERA.
Kwa upande wake Mgombea wa Urais kupiatia mwavuli wa Ukawa Edward Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anapambana katika kuondoa umasikini kwa watanzania.
“Ninagombania nafasi ya Urais kutokana na kuchoka kusikia habari ya Umasikini,nimedhamilia kupambana na umasikini,nimechoka kusikia watu wanakula mlo mmoja,nataka nikiingia tuwe tunajadili milo mitatu,ambaye ana ngombe mmoja awe na Ngombe wa wili”amesema lowassa.
Lowassa pia ameendelea kushikilia ilani yake ya elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu huku akiwapinga wanaibeza ahadi yake hiyo kwa kusema nchi hii inapesa nyingi zinazopotea kwenye Mgari ya kifahali.
  KUHUSU TANESCO.
Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha analifufua shirika la Umeme nchini TANESCO ndio litakuwa jambo lake la kwanza na kulifanya shirika hilo liondokane na mgao wa umeme.
  LEMA AFUNGUKA.
Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjinia kupitia Chadema Goodbress Lema ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC kupeleka haraka karatasi za kupigia kura kwenye mkoa wa arusha ili wananchi wawajue wagombea wao.
Amesema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo la Arusha wamezamilia kwa kauli moja kumchagua Lowassa.
written by solomon moses

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top