Wikiend iliyopita Diamond, Vanessa na Ommy Dimpoz wameiwakilisha vyema Tanzania katika tuzo za AFRIMMA zilizofanyika Marekani..Vanessa kazungumza kwenye 255 na kuwashukuru watanzania kwa kuwapigia kura, anajisikia faraja sana kushinda tuzo ya pili kimataifa, anasema imefungua kurasa mpya katika maiaha yake ya muziki.. pia amewataka wasanii wa kike wajitokeze katika sanaa hii.
Diamond baada ya kupata tuzo ya kwanza kati ya tatu alizopata aliidedicate kwa mtoto wake Tiffah..amesema ilikua ni moja ya ndoto zake na alitamani sana kupata tuzo hizo akiwa na mtoto,..jamaa anasema kuwa na mtoto kumemfanya azidi kufanya kazi kwa bidii sana ili mtoto wake aje kuishi maisha mazuri
afr
Vanessa na Diamond
Kundi la ‘mtu Chee’ linalomilikiwa na wasanii watatu Young Dee, Stamina na Country Boy limeonekana kuyumba.. kuna cover inasambaa mitandaoni ikiwa na teaser ya ngoma yao mpya lakini hayupo Young Dee na nafasi yake imechukuliwa na Young Killer..Country Boy kazungumza na kusema walikubaliana wote kutoa ngoma lakini Young Dee alionekana kutokuwa tayari na uongozi wake kumkataza kufanya kazi na kundi lake hilo..ikabidi wamuongeze Young Killer.
boy
Country Boy
Jokate na team yake ya Kidoti walifanya tour katika shule mbalimbali, Jumamosi iliyopita ilikua hitimisho la ziara hiyo katika viwanja vya Jangwani..kwenye 255 leo Jokate amesema ilifanyika Jangwani na ilikua nzuri kwa kuwa wanafunzi wengi waliitikia wito . wanatarajia kufanya kila mwaka na kutakuwa na mambo mengi mazuri zaidi.
jojo
Jokate

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top