October 7 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilishuka dimbani kucheza mechi ya hatua za awali za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018. Huu ulikuwa ni ufunguzi rasmi wa kuanza kwa hatua za awali za mechi hizo. Taifa Starsinayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa ilianza kampeni yake kwa kucheza na timu ya taifa ya Malawi.
DSC_0041
Kikosi cha Taifa Stars
Taifa Stars ambayo ilikuwa na nyota wake wote hadi wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini na Congo, imeingia ikiwa na rekodi ya kufanya vizuri katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nigeria kwa kutoka bila kufungana na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la mataifa ya AfrikaTaifa Stars katika Viwango vya FIFA ipo nafasi ya 136 wakati Malawi wakiwa nafasi ya 101.
DSC_0035
Kikosi cha Malawi
Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam imemalizika kwa timu ya taifa ya Tanzania kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0, magoli ya Taifa Starsyalifungwa na Mbwana Samatta dakika 19 na Thomas Ulimwengu dakika ya 22 . Taifa Stars itacheza mechi ya marudiano na timu ya taifa ya Malawi Jumapili ya October 11 mjini Blantyre Malawi.
DSC_0066
Mrisho Ngassa akiwania mpira na Limbikani Mzava
DSC_0058
Mbwana Samatta akishangilia goli lake akiwa na Thomas Ulimwengu
DSC_0053
Thomas Ulimwengu katika harakati za kutafuta goli
DSC_0013
Mashabiki wa Taifa Stars
DSC_0049
Shomari Kapombe akijaribu kumpita beki wa Malawi
DSC_0072
Thomas Ulimwengu akiwa chini akiugulia maumivu
DSC_0068
Thomas Ulimwengu akishangilia goli na Mbwana Samatta baada ya kufunga goli la pili
DSC_0045
Manahodha wa timu zote mbili Nadir na Mzava wakiwa na waamuzi
DSC_0003
Mashabiki wa Stars akiwa kavaa kinyago
DSC_0073
Samatta na Mzava wakiwania mpira
DSC_0075
Thomas Ulimwengu akipiga krosi wakati ambao Mivale Gabeya akijaribu kuzuia
DSC_0080
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm ni mmoja kati ya waliohudhduria mchezo huo

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top