Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefichua siku itakayomtangaza rasmi mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni Oktoba 28, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano na wawakilishi wa walemavu na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema watamtangaza mshindi wa nafasi hiyo baada ya siku tatu kuanzia siku ya kupiga kura (Oktoba 25, 2015) kwa sababu watakuwa  wameshakamilisha kazi ya kupokea na kujumlisha kura kutoka katika mikoa yote nchini.
Lubuva alieleza zaidi kuwa wamejiandaa vya kutosha na hivyo wana uhakika wa kutangaza matokeo hayo ndani ya siku tatu tofauti na ilivyokuwa katika chaguzi kadhaa zilizopita.
Mfumo wa kujumlisha matokeo utakaotumika mwaka huu (Result Management System) ndiyo unaowapa uhakika zaidi wa kukamilisha malengo yao kwani wenyewe ni maalum kwa kuondoa makosa mbalimbali ya kibinadamu yanayoweza kutokea katika ujumlishaji wa kura.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top