Siku moja baada ya msanii Nuh Mziwanda kulitaka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwa “updated” na jinsi sanaa ya sasa inavyokwenda, Baraza hilo wamemuita Nuh Mziwanda ni limbukeni kwa kutaka kuiga kisicho cha kwake.
Kauli hiyo ya BASATA imetolewa na Mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Taifaalipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari kwenye studio za East Africa Radio, na kusema kwamba asidhani kufanya muziki wa nje ndio kuwa na soko.

Huyo anayesema kitu kama hicho ana mawazo mfu, ninasema ana mawazo mfu kwa sababu ni limbukeni anataka kuiga kitu kisicho cha kwake kwa hiyo mi namwita limbukeni” alisema Maregesi.
Bwana Maregesi aliendelea kwa kusema kwamba kuiga muziki wa nje sio kuweza kupata soko, isipokuwa ni ukosefu wa elimu ya sanaa.

Asidhani kufanya muziki wa Marekani au wa Uingereza, au wa Nigeria ndiko kuwa na soko, utakuwa na soko la wapi!? Kwa sababu huwezi ukapiga muziki kuliko huyo mwenye chake, la tatu shida tuliyonayo ya wasanii wengi wa Tanzania tunafanya kazi ya sanaa bila kusomea”, aliendelea kusema Maregesi.

Pia Bwana Maregesi amewataka wasanii kuthamini kazi za nyumbani na kujikita zaidi kufanya muziki wenye asili ya Tanzania, kwani ndio utakaowapa soko kimataifa kwa utanzania wao.

BASATA iboreshe huduma zake - Nuh Mziwanda

Msanii wa Bongo Flava Nuh Mziwanda amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) kuboresha huduma zao na kuangalia jinsi tasnia ya muziki kwa sasa inavyokwenda kwani muziki huo unafanywa na vijana.

Nuh ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongokinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba lazima BASATA wawe wanakwenda na wakati na kuboresha huduma zao.

"Wale wazee ambao wako nadhani BASATA wasidhani kuwa muziki huu ni muziki ule, sasa hivi muziki umechange, wasanii wengi ni vijana sasa hivi sio wazee tena, kikubwa zaidi ni kuboresha huduma zao, kuboresha pia vitu vyao na wao pia wawe updated kwa kila kitu ambacho kinatokea sasa hivi", alisema NuhNuh pia amelipongeza Baraza hilo la sanaa Tanzania kwa kusema wanafanya kazi nzuri na kuwakumbusha wanachotakiwa kukifanya kwa maadili ya muafrika.

"Mi nawapa big up ni kazi nzuri wanaifanya wanakuwa wanatufanya sisi tunakuwa atention kuna msanii inakluwa kuna vitu vitu tunashindwa kuvifanya kwa maadili yetu waafrika", alisema Nuh.
-EATV

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top