Iran na Saudia zatupiana maneno kuhusu vifo


Image copyrightAFP
Image captionKiongozi wa kidini wa Iran , Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia msongamano wa mahujaji huko Mecca
Kiongozi wa kidini wa Iran , Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia mauwaji ya msongamano wa mahujaji huko Mecca siku ya Alhamisi ambapo zaidi ya watu 760 walifariki.
Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kiongozi huyo wa kidini, inasema kuwa jamii ya kiislamu wana maswali chungu nzima,badala ya kulaumu wengine.
Image copyrightAFP
Image captionZaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki
''utawala wa Saudia unafaa kukubali makosa na kuomba msamaha kwa jamaa ya waliuwawa au kujeruhiwa'' ilisema taarifa hiyo.
Image copyrightAFP
Image captionViongozi wa Iran wameelezea hasira zao kuhusiana na janga hilo huku wakiilaumu Saudi Arabia kwa kuongoza vibaya maeneo takatifu
Saudi Arabia tayari imekatalia mbali ukosoaji kutoka kwa Iran kuhusiana na janga hilo na kuilaumu kwa kuingiza siasa katika mkasa huo mmbaya kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu Iran kwa kujaribu kuleta siasa katika mkasa huo uliwakumba watu ambao walikuwa wakitekeleza nguzo muhimu ya kidini.
Image copyrightAFP
Image captionEneo kulikotokea maafa ya Mina
Viongozi wa Iran wameelezea hasira zao kuhusiana na janga hilo huku wakiilaumu Saudi Arabia kwa kuongoza vibaya maeneo takatifu ya ibada kwa waislamu.
Zaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top