Huwezi kuwa na urafiki na mtu anayetaka maisha yako – MeekMill amdiss tena Wale

Profile photo of sadock
Japo Boss wa Maybach Music Group, RickRoss alijaribu kulifuta bifu linaloibuka la wasanii waliochini ya label yake, MeekMill na Wale kiasi cha kutangaza ujio wa Album ya pamoja ya wasanii wa Label hiyo ‘Self Made 4′ lakini chuki kati ya wasanii hao hazifichiki.
MeekMill ametumia mtandao wa Instagram tena kutuma ujumbe wa maneno makali ambayo moja kwa moja yanaonekana yanamlenga Wale, Meek Mill ameandika “You can’t b friends with someone who want your life…. You can’t break bread with someone who want you slice…. Can’t b on a team with someone who want you to lose…. Can’t b family if it’s gotta b all about you! #MMG X #DC minus the f#%kboy.”
Wale na yeye ametumia mtandao wa Twitter ambapo amebadilisha jina na kujiita “roof whisperer” ameandika “Real Gs move in silence like Gorgonzola … Oh wait..”
Bifu la Wale na MeekMill lilianza baada ya Wale kumsifia Drake alipoulizwa mtazamo wake kuhusiana ‘MeekMill Vs Drake,’ Wale alisema Drake alienda kwenye pambano la bunduki na penseli.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top